Thursday, August 23, 2012

Mkuu Wa mkoa Wa Kilimanjaro Awapa Siku Moja Wenyeviti Wa Vitongoji Hai Kufafanua Wanataka Kufanya Kazi Za Serikali Ama La.Written by haki ngowi


Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Leonidas Gama akizungumza na wanahabari kuhusiana na maandalizi ya Sensa katika mkoa huo.
--
Na Dixon Busagaga Hai.
WENYEVITI wa vitongoji 116 katika wilaya ya Hai,wametishia kutoshiriki zoezi la sensa ya watu na makazi inayotarajia kufanyika usiku wa kuamkia Agosti 26 nchini kote kwa madai wanaidai halmashauri hiyo kiasi cha Sh Mil 280.8 ikiwa ni fedha zao za posho kuanzia mwaka 2009 hadi sasa.

Mkuu wa mkoa huo,Leonidas Gama, aliyasema hayo katika mkutano wake na wanahabari akizungumzia maandalizi ya zoezi hilo ambalo alisema limekamilika kwa asilimia kubwa .

Pamoja na kuwepo kwa tishio hilo,mkuu wa mkoa alisema wenyeviti hao wamepewa muda wa siku moja kufafanua msimamo wao iwapo wanataka kuendelea kufanya kazi za serikali ama la kutokana na kwamba madai yaohayahusiani na shughuli ya sensa.

“Kwa sasa tunachangamoto mbili kubwa, hii ya kikundi cha waislamu na hawa wenyeviti wa vitongoji wilayani Hai….nimeongea na viongozi wa wilaya yao nikawataka kama msimamo wao ni kutoshiriki zoezi hili, basiwaandike barua ya kujiondoa katika nafasi zao za uenyekiti”alisema Gama..

Aidha Gama amesema kwa mujibu uongozi wa halmashauri ya wilaya, madai ya wenyeviti hao hayakulipwa mapema kutokana na kukosekana kwa fedha katika bajeti lakini kwa mwaka huu ni miongoni mwa madai yatakayopewakipaumbele katika malipo.

Kuhusu kikundi cha waislamu wanaopinga zoezi hilo kilichopo katika wilaya za Same,Mwanga,Moshi mjini na Hai ,Gama alisema tayari jitihada zimefanyika kuwashirikisha viongozi wa madhehebu ya dini ili kuwaelimisha waumini wao kushiriki zoezi hilo.

Alisema mkoa una makarani wa sensa 4937 ambao wamegawanyika katika makundi mawili moja likiwa na makarani 2156 kwa ajili ya kujaza dodoso refu na 2279 kwa ajili ya Dodoso fupi huku makarani wa akiba wakiwa 153 na wasimamizi 349.

Akizungumzia vituo kwa ajili ya zoezi hilo alisema kuna vituo 3357 vilivyogawanywa katika makundi mawili ya Dodoso fupi vilivyopo 2279 na dodoso refu vipo 1078 na kwamba Agosti 23 imetengwa kwa ajili ya kutambua maeneo ya kazi ambapo wataongozwa na wenyeji wao ambao ni wenyeviti wa vitongoji,vijiji na mitaa.

Mkuu wa mkoa aliwataka wananchi kutunza kumbukumbu za taarifa za watu watakaolala katika nyumba zao kwa usiku wa kuamkia Agosti 26 na kwamba zoezi hilo litafanywa kwa siku saba na wasihofu iwapo makaranihawatafika tarehe 26 bali wasubiri hadi watakapofika kwa takribani siku saba

MAANDALIZI YA ZOEZI LA SENSA YAKAMILIKA MKOANI KILIMANJARO

Written by hakingowi


Mkuu wa Mkoa wa Kilimanajaro Leonidas Gama, akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu kukamilika kwa maandalizi ya Sensa ya watu na makazi ambapo pia amebainisha kuwepo kwa changamoto kubwa ya vikundi vya watu wa chache vinavyodaiwa kuwa ni vya dini ya Kiislamu,ambavyo vimeendelea na zoezi la kuwashawishiwi watu wasihesabiwe kwenye Wilayani mbalimbali Mkoani hapa.Picha na Rodrick Mushi

Ukarabati Bara bara ,Machame Mashariki


Sunday, August 19, 2012

Umuhimu wa Kituo cha kisasacha michezo Moshi

Kwa wale wanaojuwa mji wa Moshi watakubalia na wazo la kuwa na moja ya viwanja vya kisasa ,
 katika mazingira ya mkowa wa Kilimanjaro kwani yatasaidia kukuza utalii wa michezo nchini.
Pia itasaidia ushindi wa timu yetu ya Taifa na wanamichezo wa Olympic  kwa kuzingatia mazingira yenyewe yalivyo na imani ya nchi yetu kwa mlima.
Mlima kilimanjaro umekuwa ukiangaza tochi yetu ya Taifa pia kuleta sifa kemkem kuhusu nchi.
Tayari kuna mashindano ya Kilimanjaro marathoni na yakiboreshwa tunaweza kuwa na mashinda ya riadha ya ndani ya uwanja yakisindikizwa na mchezo wa mpira wa miguu.

Mfano wa kijiji cha Michezo .pic from www.webbaviation.co.uk

Leigh Sports Village -cb00276.jpg

Moshi Kilimanjaro city from the sky



Mfano wa uwanja picha kutoka www.tanzaniasports.com
TTB SPORTS OPTION CAMPAIGN MOVES TO USA
Mfano wa wanaoweza kutufadhili tuwashirikisha.
Uwanja wa http://www.soundersfc.com/