Tuesday, January 7, 2014

KILIMANJARO KUANZISHA MJI WA VIWANDA NA BIASHARA


Chanzo http://kalulunga.blogspot.se/

KILIMANJARO KUANZISHA MJI WA VIWANDA NA BIASHARA

Leonidas Gama-mkuu wa mkoa wa kilimanjaro.


 Mkoa wa Kilimanjaro unatarajia kujenga mji wa viwanda na biashara katika eneo la Lokolova ili kuchochea uongezaji thamani mazao na kukidhi mahitaji ya soko la ndani na nchi jirani.


Mkuu wa Mkoa Kilimanjaro, Bw. Leonidas Gama aliwaambia waandishi wa habari hivi karibuni mjini Moshi kuwa eneo hilo ambalo tayari limebainishwa litatoa fursa kubwa ya biashara.


“Serikali ya Mkoa kwa kushirikiana na sekta binafsi tumepanga mipango hii ili kuboresha biashara,” alisema, na kuongeza kuwa eneo hilo litajengwa viwanda vidogo, vya kati na vikubwa.


Alisema mji huo utakuwa nguzo kubwa kwa soko la kisasa la kimataifa linalotarajiwa kujengwa katika eneo hilo la Lokolova kwa ajili ya masoko ya ndani na nje ya nchi.


“Mkoa wetu huu upo mpakani na ni mashuhuri sana katika biashara lakini bado tunauza mazao ambayo ni ghafi ambayo hayana tija kubwa ya kibiashara,” alisema.


Alisema kama ilivyo katika maeneo mbalimbali nchini, bado wananchi wa mkoa huo wanauza mazao ghafi na kuwa ujio wa viwanda hivyo utasaidia kusindikwa kwa mazao hayo na hivyo kuleta tija zaidi.


Alibainisha kwamba wakati wa kuuza mazao ghafi umepitwa na wakati, hivyo mipango hiyo imekuja katika kipindi sahihi ambapo mazao yataongezwa thamani na kupangwa katika madaraja ili kupata soko zaidi.


Mkoa huo ni maarufu kwa mazao mbalimbali kama nyanya, ndizi, maparachichi na mbogamboga.


Akizungumzia mradi mwingine alisema katika wilaya ya Siha wanatarajia kuanzisha kituo kikubwa cha kisasa cha utalii ili kuongeza utalii katika mkoa wao.


“Kituo hiki kitajengwa katika maeneo yaliyokuwa ya Serikali ambayo kwa sasa hayatumiki, na kujengwa vivutio vizuri vya utalii mbalimbali,” alisema.


Kwa mujibu wa Bw. Gama, mpango huo ukikamilika utaongeza idadi ya watalii na kusaidia kukuza mapato ya sekta binafsi na umma na kukuza uchumi wa nchi.


Alifafanua kuwa vivutio vitakavyojengwa ni pamoja na eneo la maonyesho, bustani mbalimbali ikiwemo ya wanyama, maua, mahoteli ya kisasa na maeneo ya michezo.


Pia utajegwa mfano wa mlima Kilimanjaro kwa ajili ya watalii ambao hawawezi kwenda kuona na kuupanda mlima huo maarufu barani Afrika.


Alisema miradi yote hiyo itafanywa kwa ushirikiano kati ya sekta ya umma na biafsi kwa faida ya pande zote mbili.


Alisistiza kuwa mkoa wake na halmashauri zote zimebainisha maeneo ya biashara na kuyatenga ambapo sekta binafsi itayatumia kufanya biashara bila vikwazo vyovyote. 

Chanzo;michuzi blog

Thursday, December 27, 2012

SIKU YA CHAGGA YAFANA SANA MJINI MOSHI

http://michuzi-matukio.blogspot.se/

 

Tamasha kubwa la kihistoria lililopewa jina la Chagga Day Cultural Festival 2012 - Moshi lilifanyika kwenye ukumbi wa ZUMBA LAND katika manispaa ya Moshi siku ya Jumamosi tarehe 22/12/2012 kuanzia saa sita mchana mpaka saa sita usiku na kuhudhuriwa na mamia ya wakazi wa mji huo huku baadhi wakioongozana na familia zao.


Tamasha hilo lililotawaliwa na shangwe za mara kwa mara kutoka kwa wakazi wa mji wa Moshi waliofurika kwenye viwanja hivyo maarufu kwa michezo ya watoto, liliandaliwa na kampuni ya Myway Entertainment ya jijini Dar chini ya Mkurugenzi wake Paul Mganga na kudhaminiwa na kampuni ya bia (TBL) kupitia bia ya Safari Lager na kampuni ya vinywaji baridi (SBC) kupitia kinywaji chake murua cha Pepsi.

Katika shoo hiyo iliyoacha gumzo lisilokwisha kwa wakazi mjini Moshi na vitongoji vyake, kulikuwa na mambo mengi yahusuyo kabila hili maarufu ambapo historia halisi ya kabila na asili yake ilisomwa jukwaani na Mkurugenzi wa kituo binafsi cha makumbusho cha Uhuru Museum.

Tukio hilo lilikwenda sambamba na maonesho ya zana na nyenzo mbalimbali zilizokuwa zikitumiwa na wazee wa zamani wa kichagga katika kilimo, uvunaji, uandaaji vyakula, utunzaji, upishi, uhunzi, ulinzi nk huku mamia ya watu waliohudhuria walionesha kuvutiwa sana nazo na wengine wakipiga picha kwa ajili ya kumbukumbu zao.

Burudani katika shoo hiyo zilikuwa bendi ya muziki wa dansi ya Serengeti yenye maskani yake jijini Arusha, kundi la wanenguaji (dancers) wanaojiita Boda 2 Boda pia toka Arusha. Sambamba nao aliyefunga pazia la burudani alikuwa mwanamuziki wa Bongo Flava Ommy Dimpoz ambaye ali[pagawisha sana kwa nyimbo zake za Naynay, Baadae na Me & You.

Mratibu wa shoo hiyo, Paul Mganga akiongozana na Meneja wake Kaka Mwinyi, walisema kuwa, wameshukuru Mungu kwa kufanikisha onesho hilo ambalo awali lilifanyika kwa mafanikio jijini Dar es Salaam katika viwanja vya Leaders, Kinondoni miezi miwili iliyopita ambapo kama ilivyokuw Moshi, tamasha la Leaders liliburudishwa na bendi za African Stars 'Twanga Pepeta' na Msondo Ngoma.

"Hatuna cha kuongeza kwa maelezo, karibu kila kitu kimejionesha wazi... shoo imefana, watu wengi wamejitokeza, wamefurahia na familia zao kuanzia vyakula, mambo ya asili na utamaduni, muziki wa dansi, shoo za madansa, muziki wa Bongo Flava nk. Kwa ujumla timu nzima ya Myway Entertainment inawashukuru wakazi wa Moshi kwa kulipokea vizuri tamasha letu," akasema Kaka Mwinyi.

Akizungumzia mipango ya baadaye ya kampuni yake, Paul Mganga alisema kuwa, kutakuwa na mfululizo wa matamasha ya makabila mbalimbali ya Tanzania ambapo yatakayofuata ni ya kihaya, kisukuma, kinyakyusa, kingoni, kigogo, kihehe, kimakonde nk kwa lengo la kuyafikia makabila yote na kuwakutanisha wenye asili yao waburudike, waelimike na kubadilishana mawazo na mipango ya maendeleo.

mtoto akichorwa katika mashamsham ya chagga day ukumbini Zumba Land.
mkurugenzi uhuru museum akitoa historia ya kabila la wachagga.
chagga day ilivyopambwa ndani ya zumbaland mjini moshi.
boda 2 boda wakiwajibika jukwani shoo ya chagga day moshi ndani ya zumbaland.
ommy dimpoz akiimba na washabiki chagga day moshi.
ommy dimpoz akimuimbisha mtoto shoo ya chagga day ndani ya zumbaland.
thecla mgaya 'aisha' wa mambo hayo alikuwemo ndani ay nyumba akifurahia chagga day pale zumbaland moshi.
palipendezaje hapo zumbaland shoo ya chagga day.
washabiki wakiburudika na vinywaji huku wakifuatilia shoo za chagga day jukwaani pale zumbaland moshi.
akinadada hawa walikuwepo chagga day moshi.
binti huyu akikwea puto katika ukumbi wa zumbaland katika shoo ya chagga day mjini moshi.
watoto wakiinjoi kwa treni za umeme shoo ya chagga day moshi.
mfano wa santa claus akiwafurahisha watoto katika ukumbi wa zumbaland siku ya chagga day ikiwa ni maandalizi ya sikukuu ya kris
santa claus huyu alikuwepo chagga day.
zana na vifaa vya kihistoria vya wachagga vilioneshwa na uhuru museum ya moshi ndani ya chagga day moshi.

Thursday, October 25, 2012

WANANCHI WANAHAMASISHWA KUCHANGIA DAMU KWA HIARI KUOKOA MAISHA YA WAGONJWA WANAOHITAJI DAMU HOSPITALINI

  Kutoka http://www.issamichuzi.blogspot.se/2012/10/wananchi-wanahamasishwa-kuchangia-damu.html
Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro,Mh. Leonidas Gama akichangia katika kituo cha damu salama Kilimanjaro siku ya ijumaa tarehe 19/10/2012 hii ni mara ya pili mwaka huu kwa Mheshimiwa Gama kuchangia baada ya kuchangia mwezi juni 2012 wakati wa maadhimisho ya siku ya wachangia damu duniani ambayo kitaifa yalifanyika mkoani hapo. 

Mpango wa Taifa wa Damu salama Unatoa WITO kwa wananchi kujitokeza kuchangia damu kwa hiari kwenye vituo vya damu salama 
Damu ni Uhai na inahitajika, mahitaji ya damu nchini ni wastani wa chupa 400,000 kwa kipindi cha oktoba 2011- Septemba 2012 mpango umekusanya chupa 110,000.
Upungufu wa damu katika vituo vya damu salama husababisha wagonjwa kupoteza maisha kwa kukosa damu au kutopata damu kwa wakati, vifo ambavyo vinaweza zuilika kama watanzania watajenga utamaduni wa kuchangia damu mara kwa mara
Upungufu wa damu unatokana na sababu zifuatazo;
  • Uelewa mdogo wa wananchi kuhusu umuhimu wa kuchangia damu kwa hiari
  • Kuenea kwa maambukizi ya ukimwi, hivyo kusababisha watu kuwa waoga kuchangia damu
  • Uuzwaji wa chupa za damu mahospitalini kunakofanywa na watumishi wasio waaminifu hivyo kukatisha watu tama
  • Imani potofu katika jamii kuhusu uchangiaji damu Mfano uchangiaji damu unaweza kusababisha kupata maambukizi kitu ambacho si kweli
Wananchi wanaombwa kutembelea vituo vifuatavyo kuchangia damu;
 Mwanza- karibu na Hospitali ya Bugando
Tabora – karibu na Hospitali ya kitete
Dar-es-salaam- ilala mchikichini, hospitali ya lugalo, kituo kidogo cha mnazi mmoja
Mbeya- karibu na Hospitali ya Meta
Kilimanjaro- Karibu na Hospitali KCMC
Mtwara- karibu na Hospitali ya Ligula
Lindi- kituo kidogo karibu na uwanja wa ilulu
Dodoma – kituo kidogo nje ya Hospitali ya mkoa (Jenero)
Morogoro- Kituo kidogo karibu na Hospitali ya mkoa
Kagera- kituo kidogo
Na Hospitali nyingine yoyote ambayo inatoa huduma ya kuongeza damu
Kwa maelezo zaidi piga simu namba 0222181873 au 0712612000
Kumbuka; Inawezekana damu unayochangia ni kwa ajili yako, familia na jamii

Thursday, October 11, 2012

SERIKALI NA TIB ZATILIANA SAINI MKATABA WA UJENZI WA SOKO LA KIMATAIFA KILIMANJARO

 

Kutoka  MUHIDIN MICHUZI


Na Dixon Busagaga wa globu ya jamii,Moshi.


SERIKALI mkaoni Kilimanjaro na Benki ya uwekezaji nchini (TIB) zimetiliana saini ya mkataba wa mkopo wa shilingi bilioni 10 kwa ajili ya ujenzi wa soko la kimataifa la mazao ya nafaka la Lokolova, ikiwa ni hatua za awali zenye lengo la kuimarisha soko la bidhaa za ndani.



Zoezi hilo la utiaji saini lilifanywa na katibu tawala wa mkoa wa Kilimanjaro(RAS) Faisal Issa na mwakilishi wa wa benki ya TIB ,Allan Magoma katika ofisi za mkuu wa mkoa na kushuhudiwa na waziri wa jumuiya ya Afrika Mashariki Samwel Sitta, na mkuu wa mkoa Leonidas Gama .



Akizungumza mara baada ya zoezi hilo waziri Sitta alipongeza jitihada za mkoa wa Kilimanjaro, za kutafuta fedha za ujenzi wa soko hilo, ambalo litaweza kuongeza bei ya bidhaa za ndani zinazouzwa katika nchi
wanachama wa jumuiya ya Afrika Mashariki.



Waziri Sitta alisema katika shughuli za biashara kuwa na masoko ya uhakika kutasaidia kuondoa ulanguzi uliopo, na kuongeza kuwa juhudi hizo zinapaswa kuigwa na mikoa mingine kulingana na fursa zilizopo.



Alisema mkoa wa Kilimanjaro umekuwa na bahati kubwa ya kupata mkopo ambao utasaidia kuongeza tija kwa wananchi ikiwemo kukuza mapato, ya mwananchi mmoja mmoja, mkoa na taifa kwa ujumla.



Pia alisema ni wajibu wa wakazi wa mkoa wa Kilimanjaro kuanza kubuni mipango ya matumizi sahihi ya soko hilo ili kuleta faida kwa Tanzania, ikiwemo uuzaji wa mazao yenye viwango na ubora wa kimataifa, ili
kumudu ushindani.



Kwa upande wake mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro, Leonidas Gama alisema mchakato wa uanzishwaji wa soko hilo ulizingatia mahitaji na fursa za kiuchumi ambazo kwa kiasi kikubwa zina mchango kwenye kukuza pato la mkoa na taifa.



Gama alisema kwa kipindi cha mwezi Machi mpaka Julai mwaka huu pekee, serikali na wananchi wameweza kunusuru mapato makubwa ambayo yalikuwa yanapotea kutokana na wafanyabiashara kuuza mazao ya nafaka nje ya nchi kwa njia za magendo.



Kwa mujibu wake Gama, soko hilo la muda la himo, limeweza kuvusha jumla ya tani 26,585 zilizowezesha mamlaka ya mapato (TRA) kupata jumla ya dola za kimarekani 30,072 sawa na shilingi milioni 45, huku
halmashauri ya wilaya ya Moshi ikipata milioni 80 na halmashauri ya wilaya ya Rombo ikipata jumla ya shilingi milioni 21.176,.



Ujenzi wa soko hilo unazingatia maeneo kwa ajili ya maegesho, maghala ya kuhifadhi nafaka na kuwa na mashine zitakazotumika kuchambua nafaka na kuzifunga kwenye vipimo maalum tayari kusafirishwa kwenda nchi mbali mbali za Afrika Mashariki na kati.

Thursday, September 6, 2012

Wanahabari watembelea taasisi ya utafiti wa zao la Kahawa TACRI mkoani Kilimanjaro

Inatoka http://kilimanjaro-yetu.blogspot.se
Mtafiti katika taasisi ya utafiti wa zao la Kahawa Tanzania,TaCRI
kanda ya kaskazini ,John Mabagala akiwaelezea wanahabari kutoka mkoa

wa Kagera aina mpya za miche ya Kahawa ililiyo fanyiwa utafiti katika

kituo hicho.

Meneja wa programu ya uongezaji tija wa ubora wa Kahawa na msimamizi
wa maabara ya udongo TaCRI,Godsteven Maro akiwalelezea wanahabari jinsi maabara hiyo inavyo fanya shughuli zake.

Mtafiti katika taasisi ya utafiti wa zao la Kahawa Tanzania,TaCRI
kanda ya kaskazini,John Mabagala akizungumza na wanahabari kutoka

mkoa wa Kagera waliotembelea Taasisi hiyo kujionea jinsi inavyo fanya

shughuli zake.zira hiyo iliandaliwa na muungano wa vilabu nchini UTPC
na kuratibiwa na klabu ya wanahabari mkoa wa Kilimanjaro,MECKI.

Waahabari kutoka Mkoani Kagera wakiendelea kutembelea taasisi ya utafiti wa zao la Kahawa nchini TaCRI kujionea shughuli mbalimbali zinzofanywa na taasisi hiyo.

Na Dixon Busagaga waglobu ya jamii Moshi.


WANAHABARI sita kutoka klabu ya wandishi wa habari mkoa wa
Kagera(KPC)wametembelea taasisi ya utafiti wa zao la Kahawa nchini

TaCRI kujionea shughuli mbalimbali zinzofanywa na taasisi hiyo.



Ziara hiyo iliyoandaliwa na muungano wa klabu za waandishi wa habari
nchini(UTPC) na kuaratibiwa na klabu ya waandishi wa habari mkoa wa

Kilimanjaro MECKI ilikuwa na lengo la mafunzo kwa wanahabari kujifunza
na namna gani waandishi wa mikoa mingine wanavyo fanya shughuli zao
ikiwa ni pamoja na jinsi wanavyoshirikiana na wadau.



Wakiwa katika taasisi hiyo ,wanahabari hao walipata maelezo kutoka kwa
Mtafitio John Mabagala kuhusiana na shughuli zinazofanywa na kituo

hicho na baadae walipata fulsa ya kutembelea maeneo mbalimbali kituoni
hapo ikiwemo Maabara ya Udongo,Vitalu vya miche ya Kahawa na maktaba
ya taasisi hiyo.