Thursday, May 2, 2013
Thursday, April 25, 2013
Thursday, December 27, 2012
SIKU YA CHAGGA YAFANA SANA MJINI MOSHI

Tamasha kubwa la kihistoria lililopewa jina la Chagga Day Cultural Festival 2012 - Moshi lilifanyika kwenye ukumbi wa ZUMBA LAND katika manispaa ya Moshi siku ya Jumamosi tarehe 22/12/2012 kuanzia saa sita mchana mpaka saa sita usiku na kuhudhuriwa na mamia ya wakazi wa mji huo huku baadhi wakioongozana na familia zao.
Tamasha hilo lililotawaliwa na shangwe za mara kwa mara kutoka kwa wakazi wa mji wa Moshi waliofurika kwenye viwanja hivyo maarufu kwa michezo ya watoto, liliandaliwa na kampuni ya Myway Entertainment ya jijini Dar chini ya Mkurugenzi wake Paul Mganga na kudhaminiwa na kampuni ya bia (TBL) kupitia bia ya Safari Lager na kampuni ya vinywaji baridi (SBC) kupitia kinywaji chake murua cha Pepsi.
Katika shoo hiyo iliyoacha gumzo lisilokwisha kwa wakazi mjini Moshi na vitongoji vyake, kulikuwa na mambo mengi yahusuyo kabila hili maarufu ambapo historia halisi ya kabila na asili yake ilisomwa jukwaani na Mkurugenzi wa kituo binafsi cha makumbusho cha Uhuru Museum.
Tukio hilo lilikwenda sambamba na maonesho ya zana na nyenzo mbalimbali zilizokuwa zikitumiwa na wazee wa zamani wa kichagga katika kilimo, uvunaji, uandaaji vyakula, utunzaji, upishi, uhunzi, ulinzi nk huku mamia ya watu waliohudhuria walionesha kuvutiwa sana nazo na wengine wakipiga picha kwa ajili ya kumbukumbu zao.
Burudani katika shoo hiyo zilikuwa bendi ya muziki wa dansi ya Serengeti yenye maskani yake jijini Arusha, kundi la wanenguaji (dancers) wanaojiita Boda 2 Boda pia toka Arusha. Sambamba nao aliyefunga pazia la burudani alikuwa mwanamuziki wa Bongo Flava Ommy Dimpoz ambaye ali[pagawisha sana kwa nyimbo zake za Naynay, Baadae na Me & You.
Mratibu wa shoo hiyo, Paul Mganga akiongozana na Meneja wake Kaka Mwinyi, walisema kuwa, wameshukuru Mungu kwa kufanikisha onesho hilo ambalo awali lilifanyika kwa mafanikio jijini Dar es Salaam katika viwanja vya Leaders, Kinondoni miezi miwili iliyopita ambapo kama ilivyokuw Moshi, tamasha la Leaders liliburudishwa na bendi za African Stars 'Twanga Pepeta' na Msondo Ngoma.
"Hatuna cha kuongeza kwa maelezo, karibu kila kitu kimejionesha wazi... shoo imefana, watu wengi wamejitokeza, wamefurahia na familia zao kuanzia vyakula, mambo ya asili na utamaduni, muziki wa dansi, shoo za madansa, muziki wa Bongo Flava nk. Kwa ujumla timu nzima ya Myway Entertainment inawashukuru wakazi wa Moshi kwa kulipokea vizuri tamasha letu," akasema Kaka Mwinyi.
Akizungumzia mipango ya baadaye ya kampuni yake, Paul Mganga alisema kuwa, kutakuwa na mfululizo wa matamasha ya makabila mbalimbali ya Tanzania ambapo yatakayofuata ni ya kihaya, kisukuma, kinyakyusa, kingoni, kigogo, kihehe, kimakonde nk kwa lengo la kuyafikia makabila yote na kuwakutanisha wenye asili yao waburudike, waelimike na kubadilishana mawazo na mipango ya maendeleo.
mtoto akichorwa katika mashamsham ya chagga day ukumbini Zumba Land.
mkurugenzi uhuru museum akitoa historia ya kabila la wachagga.
chagga day ilivyopambwa ndani ya zumbaland mjini moshi.
boda 2 boda wakiwajibika jukwani shoo ya chagga day moshi ndani ya zumbaland.
ommy dimpoz akiimba na washabiki chagga day moshi.
ommy dimpoz akimuimbisha mtoto shoo ya chagga day ndani ya zumbaland.
thecla mgaya 'aisha' wa mambo hayo alikuwemo ndani ay nyumba akifurahia chagga day pale zumbaland moshi.
palipendezaje hapo zumbaland shoo ya chagga day.
washabiki wakiburudika na vinywaji huku wakifuatilia shoo za chagga day jukwaani pale zumbaland moshi.
akinadada hawa walikuwepo chagga day moshi.
binti huyu akikwea puto katika ukumbi wa zumbaland katika shoo ya chagga day mjini moshi.
watoto wakiinjoi kwa treni za umeme shoo ya chagga day moshi.
mfano wa santa claus akiwafurahisha watoto katika ukumbi wa zumbaland siku ya chagga day ikiwa ni maandalizi ya sikukuu ya kris
santa claus huyu alikuwepo chagga day.
zana na vifaa vya kihistoria vya wachagga vilioneshwa na uhuru museum ya moshi ndani ya chagga day moshi.
Thursday, October 25, 2012
WANANCHI WANAHAMASISHWA KUCHANGIA DAMU KWA HIARI KUOKOA MAISHA YA WAGONJWA WANAOHITAJI DAMU HOSPITALINI
Kutoka http://www.issamichuzi.blogspot.se/2012/10/wananchi-wanahamasishwa-kuchangia-damu.html
Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro,Mh. Leonidas Gama akichangia katika kituo cha damu salama Kilimanjaro siku ya ijumaa tarehe 19/10/2012 hii ni mara ya pili mwaka huu kwa Mheshimiwa Gama kuchangia baada ya kuchangia mwezi juni 2012 wakati wa maadhimisho ya siku ya wachangia damu duniani ambayo kitaifa yalifanyika mkoani hapo.
Mpango wa Taifa wa Damu salama Unatoa WITO kwa wananchi kujitokeza kuchangia damu kwa hiari kwenye vituo vya damu salama
Damu ni Uhai na inahitajika, mahitaji ya damu nchini ni wastani wa chupa 400,000 kwa kipindi cha oktoba 2011- Septemba 2012 mpango umekusanya chupa 110,000.
Upungufu wa damu katika vituo vya damu salama husababisha wagonjwa kupoteza maisha kwa kukosa damu au kutopata damu kwa wakati, vifo ambavyo vinaweza zuilika kama watanzania watajenga utamaduni wa kuchangia damu mara kwa mara
Upungufu wa damu unatokana na sababu zifuatazo;
- Uelewa mdogo wa wananchi kuhusu umuhimu wa kuchangia damu kwa hiari
- Kuenea kwa maambukizi ya ukimwi, hivyo kusababisha watu kuwa waoga kuchangia damu
- Uuzwaji wa chupa za damu mahospitalini kunakofanywa na watumishi wasio waaminifu hivyo kukatisha watu tama
- Imani potofu katika jamii kuhusu uchangiaji damu Mfano uchangiaji damu unaweza kusababisha kupata maambukizi kitu ambacho si kweli
Wananchi wanaombwa kutembelea vituo vifuatavyo kuchangia damu;
Mwanza- karibu na Hospitali ya Bugando
Tabora – karibu na Hospitali ya kitete
Dar-es-salaam- ilala mchikichini, hospitali ya lugalo, kituo kidogo cha mnazi mmoja
Mbeya- karibu na Hospitali ya Meta
Kilimanjaro- Karibu na Hospitali KCMC
Mtwara- karibu na Hospitali ya Ligula
Lindi- kituo kidogo karibu na uwanja wa ilulu
Dodoma – kituo kidogo nje ya Hospitali ya mkoa (Jenero)
Morogoro- Kituo kidogo karibu na Hospitali ya mkoa
Kagera- kituo kidogo
Na Hospitali nyingine yoyote ambayo inatoa huduma ya kuongeza damu
Kwa maelezo zaidi piga simu namba 0222181873 au 0712612000
Kumbuka; Inawezekana damu unayochangia ni kwa ajili yako, familia na jamii
Thursday, October 11, 2012
SERIKALI NA TIB ZATILIANA SAINI MKATABA WA UJENZI WA SOKO LA KIMATAIFA KILIMANJARO
Kutoka MUHIDIN MICHUZI
Na Dixon Busagaga wa globu
ya jamii,Moshi.
SERIKALI mkaoni Kilimanjaro
na Benki ya uwekezaji nchini (TIB) zimetiliana saini ya mkataba wa mkopo wa
shilingi bilioni 10 kwa ajili ya ujenzi wa soko la kimataifa la mazao ya nafaka
la Lokolova, ikiwa ni hatua za awali zenye lengo la kuimarisha soko la bidhaa
za ndani.
Zoezi hilo la utiaji saini
lilifanywa na katibu tawala wa mkoa wa Kilimanjaro(RAS) Faisal Issa na
mwakilishi wa wa benki ya TIB ,Allan Magoma katika ofisi za mkuu wa mkoa na
kushuhudiwa na waziri wa jumuiya ya Afrika Mashariki Samwel Sitta, na mkuu wa
mkoa Leonidas Gama .
Akizungumza mara baada ya zoezi hilo waziri
Sitta alipongeza jitihada za mkoa wa Kilimanjaro, za kutafuta fedha za ujenzi wa
soko hilo, ambalo litaweza kuongeza bei ya bidhaa za ndani zinazouzwa katika
nchi
wanachama wa jumuiya ya Afrika
Mashariki.
Waziri Sitta alisema katika
shughuli za biashara kuwa na masoko ya uhakika kutasaidia kuondoa ulanguzi
uliopo, na kuongeza kuwa juhudi hizo zinapaswa kuigwa na mikoa mingine kulingana
na fursa zilizopo.
Alisema mkoa wa Kilimanjaro
umekuwa na bahati kubwa ya kupata mkopo ambao utasaidia kuongeza tija kwa
wananchi ikiwemo kukuza mapato, ya mwananchi mmoja mmoja, mkoa na taifa kwa
ujumla.
Pia alisema ni wajibu wa wakazi wa mkoa wa
Kilimanjaro kuanza kubuni mipango ya matumizi sahihi ya soko hilo ili kuleta
faida kwa Tanzania, ikiwemo uuzaji wa mazao yenye viwango na ubora wa kimataifa,
ili
kumudu ushindani.
Kwa upande wake mkuu wa
mkoa wa Kilimanjaro, Leonidas Gama alisema mchakato wa uanzishwaji wa soko hilo
ulizingatia mahitaji na fursa za kiuchumi ambazo kwa kiasi kikubwa zina mchango
kwenye kukuza pato la mkoa na taifa.
Gama alisema kwa kipindi
cha mwezi Machi mpaka Julai mwaka huu pekee, serikali na wananchi wameweza
kunusuru mapato makubwa ambayo yalikuwa yanapotea kutokana na wafanyabiashara
kuuza mazao ya nafaka nje ya nchi kwa njia za
magendo.
Kwa mujibu wake Gama, soko hilo la muda la himo,
limeweza kuvusha jumla ya tani 26,585 zilizowezesha mamlaka ya mapato (TRA)
kupata jumla ya dola za kimarekani 30,072 sawa na shilingi milioni 45,
huku
halmashauri ya wilaya ya Moshi ikipata milioni
80 na halmashauri ya wilaya ya Rombo ikipata jumla ya shilingi milioni
21.176,.
Ujenzi wa soko hilo
unazingatia maeneo kwa ajili ya maegesho, maghala ya kuhifadhi nafaka na kuwa na
mashine zitakazotumika kuchambua nafaka na kuzifunga kwenye vipimo maalum tayari
kusafirishwa kwenda nchi mbali mbali za Afrika Mashariki na
kati.
Thursday, September 6, 2012
Wanahabari watembelea taasisi ya utafiti wa zao la Kahawa TACRI mkoani Kilimanjaro
Inatoka http://kilimanjaro-yetu.blogspot.se
Mtafiti katika taasisi ya utafiti wa zao la Kahawa Tanzania,TaCRI
kanda ya kaskazini ,John Mabagala akiwaelezea wanahabari kutoka mkoa
wa Kagera aina mpya za miche ya Kahawa ililiyo fanyiwa utafiti katika
kituo hicho.
Meneja wa programu ya uongezaji tija wa ubora wa Kahawa na msimamizi
wa maabara ya udongo TaCRI,Godsteven Maro akiwalelezea wanahabari jinsi maabara hiyo inavyo fanya shughuli zake.
Mtafiti katika taasisi ya utafiti wa zao la Kahawa Tanzania,TaCRI
kanda ya kaskazini,John Mabagala akizungumza na wanahabari kutoka
mkoa wa Kagera waliotembelea Taasisi hiyo kujionea jinsi inavyo fanya
shughuli zake.zira hiyo iliandaliwa na muungano wa vilabu nchini UTPC
na kuratibiwa na klabu ya wanahabari mkoa wa Kilimanjaro,MECKI.
Waahabari kutoka Mkoani Kagera wakiendelea kutembelea taasisi ya utafiti wa zao la Kahawa nchini TaCRI kujionea shughuli mbalimbali zinzofanywa na taasisi hiyo.
Na Dixon Busagaga waglobu ya jamii Moshi.
WANAHABARI sita kutoka klabu ya wandishi wa habari mkoa wa
Kagera(KPC)wametembelea taasisi ya utafiti wa zao la Kahawa nchini
TaCRI kujionea shughuli mbalimbali zinzofanywa na taasisi hiyo.
Ziara hiyo iliyoandaliwa na muungano wa klabu za waandishi wa habari
nchini(UTPC) na kuaratibiwa na klabu ya waandishi wa habari mkoa wa
Kilimanjaro MECKI ilikuwa na lengo la mafunzo kwa wanahabari kujifunza
na namna gani waandishi wa mikoa mingine wanavyo fanya shughuli zao
ikiwa ni pamoja na jinsi wanavyoshirikiana na wadau.
Wakiwa katika taasisi hiyo ,wanahabari hao walipata maelezo kutoka kwa
Mtafitio John Mabagala kuhusiana na shughuli zinazofanywa na kituo
hicho na baadae walipata fulsa ya kutembelea maeneo mbalimbali kituoni
hapo ikiwemo Maabara ya Udongo,Vitalu vya miche ya Kahawa na maktaba
ya taasisi hiyo.
Wednesday, August 29, 2012
Subscribe to:
Posts (Atom)





.jpg)
.jpg)
.jpg)