Saturday, June 30, 2012

Mazingira Kilimanjaro

Habari ya zamani,
RAIS KIKWETE AELEZEA ATHARI ZA MAZINGIRA
http://www.kilimanjaro.go.tz/kurasa/habari_moto/hm3/index1.php
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dokta Jakaya Mrisho Kikwete ametoa mifano saba ambayo ni ishara za athari mbaya zinazotokana na uharibifu mkubwa wa mazingira uliosababishwa na shughuli za binadamu.Akihutubia mamia ya wananchi kwenye siku ya Kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani ambayo kitaifa iliadhimishwa katika Uwanja wa Mashujaa katika Manispaa ya Moshi. Rais Kikwete amewataka wananchi kuchukua hatua thabiti ili kupambana na uharibifu wa mazingira.
PICHANI : Rais Kikwete akikata utepe kuzindua mradi wa upandaji wa miti wa Kanisa la KKKT Dayosisi ya Kaskazini ( Picha na Shaban Pazi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa)
Akielezea chimbuko la uharibifu wa mazingira Rais Kikwete amesema “Sisi Wanadamu tusipokuwa makini na kuchukua hatua thabiti za kutunza na kuhifadhi mazingira, uhai na ustawi wetu utakuwa mashakani ” alisema Mheshimiwa Kikwete na kusisitiza kuwa aihitaji kuwa mwanazuoni kuujua ukweli huu.
Akieleza mifano saba kati ya dalili nyingi za athari zilizotokana na uharibifu mkubwa wa mazingira ,Rais Kikwete ameanza na mabadiliko ya majira ya mwaka ambayo yamepelekea kukosekana kwa mvua za kutosha ambazo hunyesha bila ya kufuata misimu sahihi na hatimaye kusababisha ukosefu wa chakula kwani mavuno hukosekana katika kila msimu wa kilimo. Kukosekana kwa huduma muhimu zikewemo maji na umeme nayo ni moja ya majanga ambayo yameelezwa kusababishwa na ukame wa muda mrefu unaopelekea kukauka kwa vyanzo vya maji na mabwawa ambavyo ni vyanzo vya uzalishaji wa nishati muhimu ya umeme.Upungufu wa theluji katika maeneo ya ncha za Kaskazini na Ncha ya Kusini (South Pole na North Pole) za duniani ni athari ya pili kati ya athari zilizotokana na uharibifu mkubwa wa mazingira. Mheshimiwa kikwete amesma milima mikubwa yenye barafu katika maeneo haya inayeyuka. Aidha Mheshimiwa Kikwete ameeleza kuwa hata theluji iliyo kwenye vilele vya milima mikubwa duniani inayeyuka. Akitoa mifano ya milima ya Evarist , Milima ya Ulaya na hata mlima Kilimanjaro.
Kuyeyuka kwa theluji hiyo kumepelekea madhara mbalimbali katika uso wa dunia likewemo tatizo la kuzama kwa baadhi ya visiwa na kuto mfano wa kisiwa cha Mazimwi katika aneo la Pangani Mkoani Tanga kilikuwa
kikitumiwa na wanyama aina ya kasa kutaga katika eneo hilo kwa sasa kimeshazama. Mbali na hilo Mheshimiwa Kikwete amesema mji wa Pangani upo hatarini kuzama baharini na kusema kwa sasa serikali ina kazi ya kujenga ukuta ili kuunusuru mji huo ili usizame majini.Ongezeko la magonjwa nayo ni moja ya athari zilizotokana na uharibifu wa mazingira uliokithiri. Akitoa mfano wa ugonjwa malaria Rais Kikwete amesema hapo zamani ugonjwa wa malaria haukuwepo katika baadhi ya maeneo hususan yale maeneo ya miinuko ambayo hali ya hewa ilikuwa ni baridi katika majira yote ya mwaka lakini kwa sasa watu wa maeneo hayo wanasumbuliwa na ugonjwa huo kutokana na kuongezeka kwa joto Athari nyingine ni kasi kubwa ya kupungua kwa misitu hali ambayo inafanya kuongezeka kwa jangwa na kupelekea ukame kwa muda mrefu kwani mvua, mito, vijito na chemchem zimetoweka. Athari ya mwisho aliyoielezea Mhesimiwa Kikwete ni kupungua kwa ubora wa ardhi ambao hupelekea mmomonyoko wa udongo, kupungua kwa mazao ya shambani na kukosekana kwa malisho ya mifugo . Mheshimiwa Kikwete alitoa changamoto ya kupambana na athari hizo za mazingira kwa kuwataka wananchi kuchukua hatua za dhati katika kupunguza kasi ya kuharibu mazingira, kuendeleza juhudi za kujenga upya pale walipoharibu na kulinda pale palipo salama kwani chanzo kikuu cha kuharibika kwa mazingira ni jitihada za wanadamu katika kutafuta rizki na kujiletea maendeleo. Kwa mujibu wa Rais Kikwete wananchi walishindwa kuweka uwiano mzuri kati ya kile wanachochukua kutoka kwenye ardhi na kile wanachobakisha au kurudisha kwenye ardi hiyo . Aidha Mheshimiwa Kikwete ametoa pongezi kwa baadhi ya Serikali za Mitaa ambazo zimeunda kamati za mazingira zinazoratibu shughuli za usafi na utunzaji wa mazingira. Napenda kutumia nafasi hii kuzipongeza baadhi ya Serikali za Mitaa ambazo zimeunda Kamati za Mazingira ili kuratibu shughuli za kuhifadhi mazingira katika maeneo yao. Napenda kutoa mwito kwa Serikali za Mitaa ambazo bado hazijaunda Kamati hizo, wafanye hivyo mapema iwezekanavyo. Tayari nimewaagiza Wakuu wa Mikoa na Wilaya zote nchini kusimamia kwa makini Sheria na Kanuni za Hifadhi ya Mazingira katika maeneo yao. Natumaini hili litafanyika. Alisema Rais Kikwete. Rais Kikwete alitumia sherehe hizo kuzindua Kampeni ya Taifa ya Usafi na Ujenzi wa Vyoo Bora ambao unaendeshwa kwa ushirikiano baina ya Serikali, Wananchi na Washirika wa Maendeleo wa Tanzania ikiwemo Benki ya Dunia na Shirika la Umoja wa Mataifa la Mfuko wa Watoto (UNICEF). Kabla ya kufika katika uwanja wa Mashujaa Rais Kikwete alipanda Mzeituni kama ishara ya kuzindua Mpango wa Upandaji Miti wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri (KKKT), Dayosisi ya Kaskazini ambayo ina mpango endelevu wa kupanda miti kwa kuweka utaratibu wa kila mtoto atakayepokea kipaimara atatakikiwa kupanda miti kumi na kuitunza. .

No comments:

Post a Comment