Tamasha kubwa la kihistoria lililopewa jina la Chagga Day Cultural Festival 2012 - Moshi lilifanyika kwenye ukumbi wa ZUMBA LAND katika manispaa ya Moshi siku ya Jumamosi tarehe 22/12/2012 kuanzia saa sita mchana mpaka saa sita usiku na kuhudhuriwa na mamia ya wakazi wa mji huo huku baadhi wakioongozana na familia zao.
Tamasha hilo lililotawaliwa na shangwe za mara kwa mara kutoka kwa wakazi wa mji wa Moshi waliofurika kwenye viwanja hivyo maarufu kwa michezo ya watoto, liliandaliwa na kampuni ya Myway Entertainment ya jijini Dar chini ya Mkurugenzi wake Paul Mganga na kudhaminiwa na kampuni ya bia (TBL) kupitia bia ya Safari Lager na kampuni ya vinywaji baridi (SBC) kupitia kinywaji chake murua cha Pepsi.
Katika shoo hiyo iliyoacha gumzo lisilokwisha kwa wakazi mjini Moshi na vitongoji vyake, kulikuwa na mambo mengi yahusuyo kabila hili maarufu ambapo historia halisi ya kabila na asili yake ilisomwa jukwaani na Mkurugenzi wa kituo binafsi cha makumbusho cha Uhuru Museum.
Tukio hilo lilikwenda sambamba na maonesho ya zana na nyenzo mbalimbali zilizokuwa zikitumiwa na wazee wa zamani wa kichagga katika kilimo, uvunaji, uandaaji vyakula, utunzaji, upishi, uhunzi, ulinzi nk huku mamia ya watu waliohudhuria walionesha kuvutiwa sana nazo na wengine wakipiga picha kwa ajili ya kumbukumbu zao.
Burudani katika shoo hiyo zilikuwa bendi ya muziki wa dansi ya Serengeti yenye maskani yake jijini Arusha, kundi la wanenguaji (dancers) wanaojiita Boda 2 Boda pia toka Arusha. Sambamba nao aliyefunga pazia la burudani alikuwa mwanamuziki wa Bongo Flava Ommy Dimpoz ambaye ali[pagawisha sana kwa nyimbo zake za Naynay, Baadae na Me & You.
Mratibu wa shoo hiyo, Paul Mganga akiongozana na Meneja wake Kaka Mwinyi, walisema kuwa, wameshukuru Mungu kwa kufanikisha onesho hilo ambalo awali lilifanyika kwa mafanikio jijini Dar es Salaam katika viwanja vya Leaders, Kinondoni miezi miwili iliyopita ambapo kama ilivyokuw Moshi, tamasha la Leaders liliburudishwa na bendi za African Stars 'Twanga Pepeta' na Msondo Ngoma.
"Hatuna cha kuongeza kwa maelezo, karibu kila kitu kimejionesha wazi... shoo imefana, watu wengi wamejitokeza, wamefurahia na familia zao kuanzia vyakula, mambo ya asili na utamaduni, muziki wa dansi, shoo za madansa, muziki wa Bongo Flava nk. Kwa ujumla timu nzima ya Myway Entertainment inawashukuru wakazi wa Moshi kwa kulipokea vizuri tamasha letu," akasema Kaka Mwinyi.
Akizungumzia mipango ya baadaye ya kampuni yake, Paul Mganga alisema kuwa, kutakuwa na mfululizo wa matamasha ya makabila mbalimbali ya Tanzania ambapo yatakayofuata ni ya kihaya, kisukuma, kinyakyusa, kingoni, kigogo, kihehe, kimakonde nk kwa lengo la kuyafikia makabila yote na kuwakutanisha wenye asili yao waburudike, waelimike na kubadilishana mawazo na mipango ya maendeleo.
mtoto akichorwa katika mashamsham ya chagga day ukumbini Zumba Land.
mkurugenzi uhuru museum akitoa historia ya kabila la wachagga.
chagga day ilivyopambwa ndani ya zumbaland mjini moshi.
boda 2 boda wakiwajibika jukwani shoo ya chagga day moshi ndani ya zumbaland.
ommy dimpoz akiimba na washabiki chagga day moshi.
ommy dimpoz akimuimbisha mtoto shoo ya chagga day ndani ya zumbaland.
thecla mgaya 'aisha' wa mambo hayo alikuwemo ndani ay nyumba akifurahia chagga day pale zumbaland moshi.
palipendezaje hapo zumbaland shoo ya chagga day.
washabiki wakiburudika na vinywaji huku wakifuatilia shoo za chagga day jukwaani pale zumbaland moshi.
akinadada hawa walikuwepo chagga day moshi.
binti huyu akikwea puto katika ukumbi wa zumbaland katika shoo ya chagga day mjini moshi.
watoto wakiinjoi kwa treni za umeme shoo ya chagga day moshi.
mfano wa santa claus akiwafurahisha watoto katika ukumbi wa zumbaland siku ya chagga day ikiwa ni maandalizi ya sikukuu ya kris
santa claus huyu alikuwepo chagga day.
zana na vifaa vya kihistoria vya wachagga vilioneshwa na uhuru museum ya moshi ndani ya chagga day moshi.