Monday, July 30, 2012

Mama Pinda azindua mradi wa maji wa Hospitali ya Mawenzi mjini Moshi leo


   from http://josephatlukaza.blogspot.se/

Mke wa Waziri Mkuu, Mama Tunu Pinda akizindua mradi wa maji katika Hospitali ya Mawenzi pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Bia ya Serengeti anaemaliza Muda wake wa, Richard Wells. Hadi kukamilika kwa mradi huo wa maji safi, Kampuni ya bia ya Serengeti Breweries Limited imetumia zaidi ya milioni 55 za kitanzania kujenga tanki kubwa la kuhifadhi maji kwa ajili ya matumizi ya hospitali ya Mawenzi mkoani Kilimanjaro.
Mkurugenzi wa Mahusiano na Mawasiliano wa Kampuni ya bia ya Serengeti Bi. Teddy Mapunda, akifafanua juu ya gharama halisi za mradi huo.
“Sisi kampuni ya bia ya Serengeti tunatambua sana changamoto zinazowakabili watanzania, taasisi na mashirika mbalimbali hususani hospitali juu ya upatikanaji wa maji safi na salama, na kwasababu hiyo kampuni ya bia ya Serengeti imeona hilo na kuamua kusadia kutatua tatizo hilo katika maeneo mbalimbali ikianza katika maeneo yanayohitaji huduma ya maji kwa haraka zaidi” alisema Mapunda na kuongeza kuwa kujitolea kusaidia jamii ni moja yab sera za kampuni hiyo kama njia mojawapo ya kurudisha shukrani zake kwa wateja wake na watanzania kwa ujumla.

Mgeni rasmi akifungua maji yanayotoka katika bomba lililounganishwa katika matanki hayo.
Mke wa Waziri Mkuu, Mama Tunu Pinda akisalimiana na Meneja Miradi Endelevu na Uwajibikaji wa SBL, Nandi Mwiyombela
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Dkt. Mtumwa Mwako
Mkurugenzi wa Mahusiano na Mawasiliano wa Kampuni ya bia ya Serengeti Bi. Teddy Mapunda, akifafanua juu ya gharama halisi za mradi huo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Bia ya Serengeti, anaemaliza muda wake Richard Wells akizungumza wakati wa uzinduzi huo.
Baadhi ya wauguzi wa Hopitali ya Mkoa wa Kilimanjaro, Mawenzi wakifuatilia kwa umakini uzinduzi huoi.
Wadu mbalimbali nao walikuwa makini kufuatilia Matukio hayo kwa umakini.
Mkurugenzi wa Masoko wa SBL, Epraimu Mafuru akizungumza.
Mke wa Waziri Mkuu, Mama Tunu Pinda akisoma hotuba yake wakati wa uzinduzi huo wa mradi wa Maji Hospitali ya Mawenzi. Kushoto ni Mkurugenzi anaemaliza Muda wake wa Kampuni ya Bia ya Serengeti, Richard Wells baada ya kuzindua rasmi mradi huo wa maji katika Hospitali ya Mawenzi, mkoani Kilimanjaro leo.


Mkurugenzi Mtendaji wa SBL, anaemaliza muda wake, Richard Wells (kulia) akiwa na Mkurugenzi Mtendaji Mpya wa SBL, Steve Gannon, wakifuatilia hotuma ya mke wa Waziri Mkuu.
Mama Tunu Pinda akipanda mti katika hospitali ya Mawenzi mara baada ya kuzindua mradi wa maji hospitalini hapo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya SBL, Steve Gannon akimwagilia maji mti alioupanda Hospitali ya Mawenzi leo.

No comments:

Post a Comment